MPEF|Utangulizi


Kuhusu Mfuko wa Kichungaji wa Elimu Mtwara

Mfuko wa Kichungaji wa Elimu Mtwara (Mtwara Pastoral Education Fund – MPEF) ni zao la tafakari ya pamoja kati ya Jimbo Katoliki Mtwara na Chuo Kikuu Kishiriki cha Stella Maris Mtwara (STeMMUCo), SAUT MTWARA. Mfuko huo ulianzishwa rasmi tarehe 22/01/2021. Aidha, Mfuko huo umesajiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia RITA, tarehe 23/02/2022. Namba ya usajili ni 5871. Lengo la kuanzisha Mfuko huo ni kutafuta fedha kwa ajili ya kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wenye changamoto kubwa kiuchumi kutoka nchi nzima, bila ubaguzi wowote, ili waweze kupata Elimu ya chuo kwa ngazi ya Cheti, Diploma na Digrii.